MWENYEKITI wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amemshauri Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuepukana na watu wanaojiita machawa wake.
Mbowe amezungumza hayo leo Machi 8, 2023 akiwa mkoani Kilimanjaro anaposhiriki Kongamano la Siku ya Wanawake Chadema.
“Mama nakusihi katika uongozi wako ogopa sana watu wanaojiita chawa wako. Sisi kama chama kikuu cha upinzani hapa nchini tumechagua kusema ukweli bila woga, unafiki na uchawa.” Freeman Mbowe.
Mbowe amesema wao kama wapinzani wameamua kusema ukweli wakiamini ndio njia pekee ya kumsaidia Rais Samia na serikali yake.