Mbowe: Ni pigo kumpoteza Membe

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema ni pigo kubwa kwa taifa kumpoteza mwanasiasa mkongwe Bernard Membe.

Mbowe amesema  hayo alipofika nyumbani kwa marehemu Membe, Mikocheni, Dar es Salaam na kuelekeza kuwa kiongozi huyo alikuwa  jasiri na mwenye uelewa mkubwa wa masuala ya kiasa.

“Katika historia ya vyama vingi ya taifa hili, Membe anabaki kuwa kiongozi wa mfano, hakuwa mtu wa kulaumu alikuwa ni mwanasiasa mbobezi sana wa siasa wa kimataifa, Taifa limempoteza mtu muhimu sana, ” amesema Mbowe.

Habari Zifananazo

Back to top button