Mbunge agawa mitungi 300 ya Gesi kwa makundi mbalimbali

KAGERA, Bukoba,Mbunge wa Viti maalum kupitia asasi zisizo za  kiserikali  NGO,s Neema Lugangira amezindua Kampeni  ya  “Pika kwa Gesi, tunza mazingira”inayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kampeni hiy ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo aliyotoa Rais Dk Samia Suluhu Hassan wakati wa Kongamano la nishati Safi ya Kupikia lililofanyika tarehe 1 Novemba 2022, Dar es Salaam.

Kampeni ya Pika kwa gesi, tunza mazingira inaratibiwa na Ofisi ya Mbunge Lugangira kupitia Neema na Maendeleo na Shirika la Agri Thamani ambalo Mbunge  huyo ni Mkurugenzi na mwanzilishi wake.

Kampeni hii imeanzia Wilaya ya Bukoba mjini ikifuatiwa na Wilaya ya Muleba na inatarajiwa kufiki maeneo mengine ndani na nje ya Mkoa wa Kagera kulingana na uwezeshwaji utakaopatikana.

Kupitia uzinduzi wa kampeni ya Pika kwa gesi, tunza mazingira jumla ya mitungi 300 ya gesi imetolewa kwa viongozi wa makundi mbalimbali, wajasariamali, mama lishe na watu Mashuhuri katika Wilaya ya Bukoba mjini kama sehemu ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati salama.

Habari Zifananazo

Back to top button