Mbunge ahoji kigezo cha kuandika mtihani kujiunga VETA

DODOMA; MBUNGE wa Viti Maalum, Rose Tweve, amehoji bungeni kaa kigezo cha mtihani wa kuandika kabla ya kujiunga na Vyuo vya Ufundi (VETA) ni cha lazima kwa wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga, amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), inatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa nadharia kwa asilimia 30 na vitendo kwa asilimia 70.

‘’Kwa kutambua umuhimu wa Stadi za Kuandika, Kusoma na kuhesabu (KKK) katika utoaji wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA hutoa Mitihani ya Majaribio (Aptitude Test) wa kujiunga kwenye vyuo vyake.

‘’Hii ni kwa sababu kuna umuhimu wa kubaini endapo wanaotaka kujiunga na Vyuo vya VETA wanamudu stadi za KKK ikiwa ni kigezo cha kujiunga na vyuo vya ufundi stadi na pia kwa ajili ya muendelezo wa kielimu kwa hapo baadae pindi mwanafunzi akihitaji kujiendeleza zaidi,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button