Mbunge akataa ‘English Medium’ za Serikali

TASKA Restituta Mbogo, Mbunge wa Viti Maalum ameshauri Lugha ya Kiingereza ifundishwe kuanzia darasa la kwanza katika shule zote za serikali kwa lengo la kuondoa matabaka ndani ya jamii.

Akitoa mchango wake kwenye hotuba ya bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, Jumanne, Mbunge huyo amesema si sahihi kwa walimu wanaolipwa na Serikali kwenda kufundisha shule zinazotumia mchepuo wa Kiingereza zilizojengwa na halmashauri.

Amesema kuwa hakubaliani amesema shule hizo zimejengwa kwa fedha zinazokusanywa kutoka kwa wananchi kisha wanaoweza kusoma hapo ni wenye uwezo pekee.

Advertisement

Licha ya kusema kuwa hakubaliana na hali hiyo, Mbunge huyo amesisitiza: “Hali hii itajenga matabaka. Yule mtu uliyemchukulia hela yake; dereva bodaboda, muuza mitumba hawezi kumleta mtoto wake pale.”

Suluhisho la jambo hilo, Mbunge ameeleza, somo la Kiingereza linatakiwa lifungishwe shule zote za umma kuanzia darasa la kwanza ili kuleta usawa katika jamii.

Mbali na suala la lugha ya kufundishia, wabunge waliopata fursa ya kuchangia bajeti hiyo wameitaka serikali kuweka mkazo katika ujuzi ili wahitimu waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali. Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara ameitaka Serikali kuondoa kero katika sekta hiyo.