Mbunge alia na mabilioni ya wamachinga

DODOMA; Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Saidi Lulida (CCM), amehoji fedha zinazokusanywa za wamachinga zinakwenda wapi na kuongeza kuwa mpaka sasa hakuna takwimu sahihi zinazoonesha kuna wamachinga wangapi nchini.

Mbunge huyo amesema hayo bungeni wakati akichangia mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2023 iliyowasilishwa leo Februari 7, 2024 mjini Dodoma.

Amesema kuna wingi wa Wamachinga wanaofanya biashara ndogo, lakini hawana vitambulisho huku kila siku wakitozwa Sh 1000, ambayo ni sawa na Sh 30,000 kwa mwezi ambazo ni takriban Sh 360,000 kwa mwaka kwa kila mmachinga mmoja, huku akisikitika kuwa hizo ni fedha nyingi sana kwa idadi ya wamachinga wanaofanya biashara na hazijulikani zinakwenda wapi.

Advertisement