Mbunge alia na mafao kwa wastaafu

DODOMA; Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Ester Bulaya, amesema bado kuna malalamiko mengi ya watumishi wa umma kuhusu malipo ya mafao yao kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSSSF.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma wakati akichangia bajeti ya maakadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2024/2025 Ofisi ya Waziri Mkuu, Bulaya amesema serikali inapaswa kukaa chini na kupitia upya stahiki za malipo ya wastaafu, ili mgawanyo wa malipo ya wastaafu katika vikokotoo uweze kuwanufaisha kulingana na utumishi wao.

Amesema licha ya jitihada zinazowekwa na serikali kutumia fedha mfuko huo kwa ajili ya uwekezaji, lakini bado hakuna mafanikio yoyote katika kulinda maslahi ya wastaafu wa serikali.

“Tunajua adha wanapata wstaafu wetu sote tunajua kikokotoo bado ni janga na hii haijaisha mpaka iishe, ilianza kulalamikiwa tangu sheria ilivyotungwa hitaji yao ilikuwa asilimia 50 mkaleta asilimia 33, lakini bado kuna malaalmiko ya watumishi,” amesema Bulaya.

Habari Zifananazo

Back to top button