Mbunge aliyekufa kwa trekta kuagwa kesho

MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali (CCM), Francis Mtega (54) aliyekufa kwa ajali ya pikipiki Julai Mosi mwaka huu unatarajiwa kuagwa kesho nyumbani kwake Chimala mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, kikao cha familia kimekubaliana baada ya mwili huo kuagwa utasafirishwa kwenda Kijiji cha Lugalawa wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe kwa ajili ya mazishi na maziko yatakayofanyika Jumatano kijijini hapo.

Mtega alipoteza maisha baada ya kugongwa na trekta akiwa anaendesha pikipiki yake akienda shambani kwake. Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni Chimala, Dk Peter Kigombola alisema kiongozi huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba walipomfanyia uchunguzi wa awali walibaini kuwa alikua tayari ameaga dunia.

“Tulipouchunguza mwili huo tulibaini kuwa ulikua na majeraha kichwani, mgongoni na tumboni inasemekana baada ya kugongwa na lile trekta lilimpitia tena mgongoni,” alisema Dk Kigombola.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Denis Mwila alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la kibaoni, Tarafa ya Ilongo, Kata ya Chimala. Mwila alisema ajali hiyo ilihusisha trekta lililokuwa likiendeshwa na Alex Kibega (18), mkazi wa Kibaoni likitoka Kapunga kwenda Chimala.

Trekta hilo lilimgonga mbunge huyo aliyekuwa akiendesha pikipiki namba MC 573CGT aina ya Boxer na kumsababishia kifo. Mwila alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Kibega kutokuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara Mbunge huyo aliyezaliwa Juni Mosi mwaka huu alichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Mbarali mwaka 2020.

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha mbunge huyo. Kupitia akaunti yake katika mtandao wa kijamii wa twitter Rais Samia alisema Mtega atakumbukwa kwa jitihada zake kuwatumikia wananchi wa Mbarali na miaka yake ya utumishi katika sekta ya afya. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema Bunge limepokea kwa maskitiko kifo cha Mtega.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Francis Mtega. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Jimbo la Mbarali. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na Subira katika kipindi hiki kigumu,” alieleza Dk Tulia kupitia taarifa ya kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha bunge.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kim
Kim
2 months ago

My last paycheck was $2500 for working 12 hours a week online. My sisters friend has been averaging 8k for months now and she works about 30 hours a week. I can’t believe how easy it was once I tried it out. The potential with this is endless.

This is what I do……….>>> https://goodfuture10.blogspot.com

Last edited 2 months ago by Kim
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x