Mbunge apongeza uimarishwaji vifaa tiba Hospitali ya Rufaa Morogoro

MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ameipongeza serikali kwa kuipatia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa mashine ya CT- Scan ya kisasa.

Hatua hiyo inafanya wananachi kupata huduma hiyo pasipo kusafiri tena kwenda Hospitali ya Muhimbili na nyinginezo Dar es Salaam.

Abood ametoa pongezi na shukrani hizo Desemba 29, 2023 alipozindua a na kupokea magari mawili, moja lililotolewa na Wizara ya Afya kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo na lingine lililonunuliwa na hospitalk hiyo kutokana na mapato yake ya ndani .

Mbunge Abood amesema Serikali imewezesha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo kuwa na uwezo mkubwa wa utoji wa huduma kutokana kuwepo kwa vifaa vya kisasa vinavyosaidia kuokoa uhai wa wananchi wanaopatwa na magonjwa mbalimbali.

“Sasa wananchi wengi wa Morogoro wahaendi tena nje ya mkoa na wanapata huduma yao kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wao” amesema Abood.

Abood  amewapongeza madaktari na wauguzi kutokana na kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ya kuwahudumia wananchi kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo.

“ Ninawahakikishia nitaendelea kuiomba serikali sikivu kuongeza vifaa ambavyo vimepungukiwa ili kuwa na utosherevu utakaowezesha kufanya majukumu yenu vizuri zaidi ya kuwahudumia wananchi kuweza kupata hduma bora za afya” amsema Abood.

Mbunge Abood alimpongeza Serikali kwa kuipatia Hospitali hiyo gari kwa ajili ya shughuli za kiutawala ambalo litasaidia madaktari kuwahudumia wananchi wa wilaya zote za mkoa huo.

“ Mimi naendelea kuipongeza serikali ya awamu ya sita mama yetu Samia Suluhu Hassan na tunamwombea afya njema na tunampa tena mitano mingine …maana serikali hii ni ya vitendo si ya maneno na sisi tukiwa wabunge tutaendelea kumshauri na kulishauri Bunge kwa manufaa ya wananchi “ amesema Abood.

Kwa upande wake , Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk Daniel Nkungu , amesema gari hilo ni sehemu ya majibu ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kufuatia hoja na ombi la Wabunge walilolitoa Bungeni kwa Serikali.

“ Tunakushukuru Mbunge na wabunge wenzako katika mikoa mingine yote ya Tanzania kwa sababu magari haya tusigeyapata endapo msingetusemea kule Bungeni ‘ amesema Dk Nkungu

“ …Tumepokea gari kutoka wizara ya Afya kwa maana ya mgao wa serikali nah ii ni kutokana na juhudi Morogoro mitano tena kwa Rais Dk Samia.”

Habari Zifananazo

Back to top button