Mbunge asifu miundombinu Msomera

MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Ngorongoro ,Kaika Saning’o ole Telele, amesema serikali imeweka miundombinu ikiwemo majosho, barabara na mawasiliano kwa wananchi waliohamia kwa hiyari Msomera wilayani Handeni, wakitokea Hifadhi ya Ngorongoro.

Telele ametoa shukrani hizo wakati akizungumza na wanahabari juu ya utofauti kati ya mazingira ya awali waliokuwa wakiishi Ngorongoro na hali halisi ya Msomera baada ya kuamua kuondoka.

Kaika Saning’o ole Telele,

Anasema miundombinu ya barabara za changarawe,huduma za mawasiliano ya simu, sanjari na uhuru wa kufanya shughuli mbalimbali ndio maendeleo makubwa kwa wananachi waliokuwa wakitamani kuyapata.

“Nimehamia hapa na mifugo yangu na hivi sasa najenga nyumba ya kisasa zaidi ya hii niliyopewa na serikali, hapa mawasiliano ya simu nayapata, barabara nzuri,huduma za mifugo na nyingine za kijamii nazipata, kweli Msomera ni pazuri fursa za mawasiliano zimejaa tele tofauti na kule tulipokuwa awali,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button