BAADA ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutoa tiketi 5000 kwa ajili ya kuiona Yanga dhidi ya USM Alger mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho, viongozi wengine wamehamasika na wameendelea kufuata nyao hizo.
Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM) Abdulaziz Abood amenunua tiketi 1,000 kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa Mei 28, 2023, Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.
Mashabiki wa Yanga kutoka Morogoro wamempongeza mbunge huyo kwa uzalendo aliouonesha mbunge huyo.
Mchezo huo utakuwa wa mkondo wa kwanza na baada ya hapo Yanga wataenda *Algeria* kwa ajili ya fainali ya mzunguko wa pili.
Comments are closed.