Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mshariki EALA, James Ole Millya amempongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kutoa ardhi kwaajili ya kuimarisha kamisheni ya kiswahili Zanzibar na kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EAC) kwaajili ya ujenzi wa makazi.
Millya amesema hayo nje ya Bunge la Jumuiya hiyo wakati wa uwasilishwaji wa makadirio ya bajeti ya dola za marekani. 103,842,880 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,Vijana,Michezo na Utamaduni wa Burundi, Balozi, Dkzechiel Nibagira ambaye amesema makadirio ya bajeti hiyo ya mwaka 2023/24 .
Amesema Rais Samia ametoa zaidi ya ekari 100 kwaajili ya taasisi mbalimbali za kiswahili Zanzibar ikiwemo makazi kwa watu mbalimbali wa EAC
Lakini pia masuala ya amani kwa nchi za EAC haswa Mashariki ya Kongo ikiwemo uwekaji wa miradi mbalimbali
“Nampongeza Dk,Samia kwa kutoa ardhi kwaajili ya kamisheni ya kiswahili sanjari na makazi ya wanachama wa EAC lakini naiona Jumuiya bora zaidi kwasababu ya nguvu ya pamoja na anaendelea kuishi njozi za hayati Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wakuu zikiendelea kuishi”
Naye Mbunge wa EALA kutoka nchini Kongo, Masirika Ngaiza Dorothee amesema kuwa bajeti hiyo inamambo mengi na itasaidia kuipeleka jumuiya mbele katika mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya afya,elimu na kuomba nchi wanachama kuchangia zaidi michango yao ili kuongeza ufanisi zaidi katika bajeti na kazi nyinginezo ziendelee.