WANAWAKE wajasiriamali 400 kutoka Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wamepatiwa majiko ya gesi 400 kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Majiko hayo kutoka kampuni ya Lake gas yametolewa na mbunge wa jimbo la Ilemela, Dk Angeline Mabula wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Halamshauri ya Ilemela.
Dk Angeline Mabula ametoa mitungi ya gesi mia 900 mwezi juni alitoa mitungi 500 na mwezi desemba ametoa mitungi 400 Kwa akina mama wajasiriamali Ili kumpunguzia mama mzigo WA kuhangaika kutafuta mkaa au kuni kwani huchukua muda.
Amesema mipango ya Rais Samia Suluhu ni kuinua wananchi wenye kipato cha chini kwani anamgusa kila mwananchi.
“Kama huwezi kupangilia ratiba yako vizuri huwezi kufanikiwa panga vizuri kwasababu wewe ndio utakaejua chakula kimepikwaje,je tunakula vya mchemsho kwahiyo tutumie fursa hiii ya kutumia nishati safi Ili kufanya mambo Kwa wakati .” aliseman Dk Mabula.
Ameongeza kuwa lengo la Rais Samia Suluhu ifikapo 2032 Watanzania wote hususani akina mama lishe waondokane na nishati zinazodhuru afya zao na kupoteza muda wa utendaji kazi wao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amesema kuwa kundi la wanawake ni muhimu sana hivyo kuna uhitaji mkubwa wa uwekezaji wa vitendea kazi vyao.
Masala amesema kuwa Ilemela itaendelea kumuunga mkono rais Samia kwa kutumia nishati mbadala kwa wanawake.
Mkazi wa mtaa wa Igogo wilayani Ilemela Frozia Paulo amesema nishati hiyo itamsaidia kupunguza gharama kutokana na mkaa kuwa bei ya juu. Alisema jiko aliopewa litaimarisha utendaji kazi wake na amemshukuru Mbunge wa jimbo la Ilemela Dk Angeline Mabula.
Katika kipindi cha mwezi Juni mpaka Septemba mwaka huu Dk Mabula jumla ametoa majiko ya gesi 900 mitungi ya gesi 900 kwa wanawake wajasiriamali 900 wa manisapaa ya Ilemela.