Mbunge Salim Hasham awapa neno wanafunzi wa vyuo Morogoro

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Hasham

MOROGORO: WANAFUNZI zaidi ya 20,000 kutoka katika vyuo mbalimbali mkoani Morogoro wamekutanishwa kujengewa uwezo wa kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa ajira baada ya kuhitimu masomo yao.

Akizungumza na wanafunzi hao mkoani humo mapema leo, Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Hasham amewataka vijana hao kupenda fani wanazosomea ili kupata mafanikio.

“Tuna upungufu wa ajira, lakini hatuna upungufu wa kazi, kila siku lazima ubuni kitu kipya,” amesema mbunge huyo.

Advertisement

Mariam Mika mwanafunzi kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari Mogorogo (MSJ) na Elia Ngachucha kutoka St Joseph College mara baada ya kupatiwa elimu hiyo wameshukuru kwa kupewa nafasi hiyo na kuomba wahusika kuendelea kuwaelimisha zaidi.