Mbunge: TRA ni wavivu wa kufikiri

DODOMA; Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole, amesema Wizara ya Fedha kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ni wavivu wa kufikiri.

Akichangia bungeni leo Juni 4, 2024 hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Mbunge huyo amesema badala ya TRA kufikiria vyanzo vipya vya mapato inakamua wakulima kwa kuwataka wawe na mashine za kielektroniki (EFD).

Amesema si sahihi wakulima kutumia EFD, kwani wao sio wafanyabiashara badala yake wanalipia ushuru, lakini kuwalazimisha watumie mashine hizo ni kuwaonea.

Wakati Mbunge huyo akichangia, Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba alisimama kutoa taarifa kwa mchangiaji kwa kueleza kuwa TRA si wavivu wa kufikiri, kwani wao hawatungi sheria badala yake wanatekeleza sheria zilizotungwa na Bunge.

Amesema wabunge kama kuna sheria wanafikiri haifai waeleze ifanyiwe kazi, badala ya kusema TRA ni wavivu wa kufikiri. Mbunge alikataa kupokea taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button