Mbunifu wa mavazi awa kivutio jukwaani

MBUNIFU wa mavazi mahiri nchini, Kiki Zimba amekuwa gumzo kwenye Onesho la Mitindo la Swahili Fashion 2022 hasa kutokana na ubunifu wa vazi lake lililoonesha Mlima Kilimanjaro ambalo lilivutia wageni wengi.

Kama ilivyo kawaida yake ya kufanya onyesho siku ya tatu ambayo ni siku ya mwisho ya onesho hilo la siku tatu siku ambayo wabunifu mahiri ndiyo ufunga shoo wanamitindo waliovalia mavazi ya mbunifu huyo waaliingia kwenye Run Way wakiwa na mavazi ya aina mbalimbali.

Wanamitindo hao walionesha mavazi mbalimbali yakiwemo ya kutokea kwenye dhifa za kila aina, baada ya kuonesha mavazi hayo ndipo akaingia mwanamitindo aliyevalia vazi hilo la Mlima Kilimanjaro ambalo liliwavutia wageni wengi na wengine wakijikuta wanapiga makofi ya kumpongeza Kiki.

Akizungumzia kuhusiana na vazi hilo, Kiki anasema ”dhumuni la kubuni vazi hili ni kuutangaza Mlima Kilimanjaro kwa kuwa mwezi Septemba mwaka huu nilipanda na kujikuta nikivutiwa na mazingira ya Mlima huo yani hata watalii wanaupenda sana ndo maana ujumbe wangu kupitia fashion hasa kwenye Swahili Fashion 2022 ni kuwataka watanzania na wageni kuupanda” anasema Kiki.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x