Mbwana Makata kocha mpya Ruvu Shooting

KLABU ya Ruvu Shooting imemtangaza Mbwana Makata kuwa kocha wao mpya akisaini mkataba wa mwaka mmoja na kuchukuwa nafasi iliyoachwa na Charles Mkwasa.

Ruvu imelazimika kumtangza kocha huyo kuziba nafasi hiyo iliyoachwa na Mkwasa aliyetangaza kujiuzulu jana kutokana na matokeo mabovu yanayoikumba timu hiyo.

Makata aliwahi kuifundisha Mbeya Kwanza na Dodoma Jiji.

Mpaka sasa timu hiyo imecheza michezo 15, na kujikusanyia pointi 11, kwa takwimu hizo timu hiyo inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu.

Habari Zifananazo

Back to top button