MC Zuzu amlilia Sauti ya Kiza
DAR ES SALAAM: MSANII wa hip hop na mwanaharakati wa Lugha ya Kiswahili nchini, Mutalemwa Jason Mushumbusi maarufu Maalim Nash ‘MC Zuzu’ ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha gwiji wa Kiswahili na Ushairi nchini, Amiri Sudi Andanenga.
Akitumia mitandao yake ya kijamii @maalimnash leo amechapisha andiko lenye kichwa ‘KISWAHILI KIMEFIWA’.
https://www.instagram.com/p/C6a_KNKoioK/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
“Gwiji wa ushairi maarufu kwa jina la SAUTI YA KIZA. Kwa wapenzi na wakereketwa wa Kiswahili bila shaka tumepata pengo kubwa sana,” amesema Nash.
Katika maelezo yake, mtunzi huyo na mwimbaji wa Albamu ya Mhadhiri ameeleza kuwa Sauti ya Kiza atazikwa leo katika makaburi ya Kinondoni.
“In Shaa Allah, Mwenyezi Mungu amhifadhi,” ameeleza msanii huyo.