Mchengerwa aja na majibu ya changamoto ya eneo la Jangwani

DAR ES SALAAM; WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa leo Novemba 13, 2023 ametembelea eneo la Jangwani Jijini Dar es salaam ambapo kutokana na eneo hilo kukumbwa na Mafuriko ya mara kwa mara amesema kuwa mapema mwakani ujenzi wa daraja kubwa utaanza kufanyika na kwamba kinachoendelea ni mashauriano ili ujenzi huo kuwa na ufanisi zaidi.

Pia Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya nchini kuhakikisha wana wasaidia Wananchi waliokumbwa na Mafuriko katika maeneo mbalimbali badala ya kukaa ofisini.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewataka Watendaji wa Wakala wa Barabara Tanroad na Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) kutoka Ofisini na kufanya mapitio ya barabara kipindi hiki cha mvua huku akimsisitiza Meneja wa TANROAD Mkoa wa Dar es salaam kuondoa tope lililopo chini ya daraja hilo la Jangwani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema zoezi la kuondoa mchanga linaendelea kama hatua za muda mfupi huku Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROAD ,Mhandisi Dorothy Mtenga na Mratibu wa Mradi kutoka Benki ya Dunia, Injinia Humphrey Kanyenye wakisema ujenzi wa eneo hilo utahusisha utunzaji wa mazingira.

 

Habari Zifananazo

Back to top button