WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa ameridhia uteuzi wa Mabula Misugwi kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA).
Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha mawasiliano Wizara ya Maliasili iliyotolewa leo Machi 5, 2023 imemnukuu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Hassan Abbasi kuwa uteuzi huo unaanza leo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuz huo ni kwa mujibu wa aya ya 3.
1.2 ya amri ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania.