Mchengerwa ataka Mganga Mkuu Kagera kusimamishwa

KAGERA: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amemwagiza katibu Mkuu TAMISEMI kutengua nafasi ya Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Kagera, Issesanda Kaniki baada ya kupata malalamiko mbalimbali kuwa huduma na lugha zinazotolewa katika zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba haziridhishi.
Mchengerwa amesema amechukizwa na malalamiko ya mara kwa mara yanayotoka kwa wananchi na kufika ofisini kwake juu ya watumishi na viongozi wa hospitali hiyo kuwa na lugha ya matusi na kutoa huduma zisizofaa.
Ameongeza kuwa hivi karibuni amepokea malalamiko ya mwanamke mmoja aliyefiwa na mtoto mchanga na maiti ya mtoto huyo ikazuiliwa siku mbili kwenda kuzikwa huku viongozi na watumishi wote wa afya wakijua kuwa gharama za matibabu kwa watoto wachanga ni bure.
Aidha amesema kuwa serikali haitamvumilia mtumishi ambaye hawezi kufanya vizuri katika nafasi yake hivyo watumishi wanapaswa kujitafakari kwani atayeshindwa kutumikia nafasi yake atavuliwa cheo chake kwani muda wa mazoea kazini umesha pitwa na wakati.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button