Mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa waahirishwa

BODI ya Ligi Kuu (TPLB) imeahirisha mchezo wa Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kuchezwa Jumapili Februari 18, 2024 uwanja wa Jamhuri ,Morogoro.

Taarifa iliyotolewa leo Februari 16 na bodi hiyo, imeeleza sababu za kuahirisha mchezo huo ni kutoa nafasi kwa Simba kufanya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba italazimika kusafari kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa ligi hiyo hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas mchezo utakaofanyika Ijumaa ya Februari 23.

Advertisement

TPLB imeeleza kuwa mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine hivi karibuni