Mchungaji Kimaro aaga waumini KKKT Kijitonyama

MCHUNGAJI Dk Eliona Kimaro wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama ameaga waumini wa kanisa hilo kutokana na kuanza likizo ya siku 60.

Akiaga waumini jana Januari 16, 2023 katika semina ya maombi na mfungo wa siku 14 uliopangwa kuanza leo, Mchungaji Eliona aliaga waumini na kudai kuwa amepewa barua ya likizo kwa siku 60 na zitakapoisha atatakiwa kurudi Dayosisi na sio usharika wa Kijitonyama.

“Kuanzia kesho (leo) Mchuangaji Anna ataendelea kuwa mchungaji wa usharika huu, naomba muendelee kumpa ushirikiano, ” alisema Mchungaji Dk Kimaro na kuongeza kuwa:

“Mimi ni Mchungaji wa Lutheran ninayeheshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo changu cha kichungaji na maadili pia ya kichungaji kwa neema ya Mungu.

“Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyoelekezwa asante, ” alisema Kimaro akiaga.

Habari Zifananazo

Back to top button