Mchungaji: Nilifungwa jela miaka 5 kimakosa

MOROGORO; Gairo. Tume TUME ya Utumishi wa Mahakama Tanzania imeombwa kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wananchi hasa waishio vijijini juu ya namna ya kuwasilisha malalamiko yao katika kamati za maadili za maofisa mahakama nchini.

Uwasilishaji wa malalamiko hayo ni pale wanapofanyiwa vitendo vinavyokiuka kanuni za maadili, ili haki zao zilindwe na kupata haki kwa wakati.

Mchungaji wa Kanisa la Anglikana wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Canon Benedict Mbelwa ametoa ombi hilo mjini Gairo wakati wa mkutano wa utoaji wa elimu ulioendeshwa na viongozi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania.

Utoaji wa elimu kwa wananchi wa Gairo uliongozwa na Naibu Katibu Maadili na Nidhamu wa tume hiyo, Alesia Mbuya pamoja na Naibu Katibu wa Tume (Ajira na Uteuzi ) , Enziel Mtei na kumshirikisha Mkuu wa wilaya hiyo, Jabir Makame.

Licha ya kuwasilisha ombi hilo, Mchungaji huyo ameeleza namna alivyoingizwa katika kesi isiyomhusu na kuhukumiwa kifugo cha miaka mitano jela na wenzake wawili katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuchanguliwa kuongoza Saccos ya Mshikamano.

Mbelwa amedai alishitakiwa bila sababu yoyote na kufungwa miaka mitano na Mahakama ya Mwanzo ya Pandambili iliyopo Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma kwa kesi iliyofunguliwa ya Mshikamano Saccos.Amedai waliokuwa viongozi wa bodi kwa wakati huo walifanya ‘madudu’ na wao walipochanguliwa waliamua kuangalia kilichofanyika katika Saccos hiyo ,lakini ghafla walifunguliwa kesi bila ya kuelewa mazingira yake.


“ Nililala rumande siku sita , baadaye nikadhaminiwa na hata uendeshaji kesi yenyewe haukuwa wa uwazi, nikahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na kuipata ile nakala ya hukumu ilichukua muda mrefu, “amedai Mchungaji Mbelwa.

Mchungaji Mbelwa amedai walipewa haki ya kukata rufaa ,na kutokana na juhudi za Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Morogoro alimpatia mwanasheria wa Dayosisi kuweza kusimamia rufaa yao.

“Tulifungwa miaka mitano jela mimi na wenzangu wawili , baada ya kushinda rufaa tukaachiwa wawili , isipokuwa mmoja wetu bado anaendelea kutumikia jela,” amebainisha Mchungaji Mbelwa.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
CharleeJewell
CharleeJewell
2 months ago

[ JOIN US ] I am making a good salary from home $16580-$47065/ Dollors week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. ( i72q) I thank God every day I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started.…………> http://Www.SmartCareer1.com

JenniferGale
JenniferGale
2 months ago

I’ve got my first check for a total of 13,000 dollars. I am so energized, this is whenever I first really acquired something. I will work much harder now and I can hardly hang tight for the following week installment.
.
.
Detail Here…………………………………………………………….. http://Www.BizWork1.Com

KaliMcDougall
KaliMcDougall
2 months ago

I even have made $17,180 only in 30 days straightforwardly working a few easy tasks through my PC. Just when I have lost my office position, I was so perturbed but at last I’ve found this simple on-line employment & this way I could collect thousands simply from home. Any individual can try this best job and get more money online going this article…..
>>>>>   http://Www.Careers12.com

Last edited 2 months ago by KaliMcDougall
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x