SINGIDA: Baada ya mchezo wa leo kumalizika kwa sare Simba sasa wamecheza michezo minne bila kupata ushindi.
Simba walipoteza bao 1-0 kutoka kwa Al Ahly Uwanja wa Benjamini Mkapa, kisha wakafungwa 2-0 na Al Ahly nchini Misri katika Ligi ya Mabingwa Afrika, baadae walirejea nyumbani na kusambaratishwa kwenye Kombe la Shirikisho la CRDB na Mashujaa FC , na leo wameshikwa shati na Ihefu kwa sare ya 1-1.
Simba imefikisha alama 46 lakini bado inaendelea kusalia katika nafasi ya tatu kwenye msimamo huku Ihefu wakifikisha alama 24 katika nafasi ya tisa.
Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga mnamo Aprili 20, Uwanja wa Benjamini Mkapa.