Mechi ya KMC v Yanga saa 10 alasiri

Mayele

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga SC na KMC utapigwa saa 10:00 alasiri katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, badala ya saa 1:00 usiku.

Taarifa hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mchezo huo utakuwa wa raundi ya 23 kwa timu zote mbili, ambapo timu hizo zitakuwa zimebakisha michezo saba kila moja kumaliza ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.

Advertisement

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *