Mechi ya Simba vs Yanga yasogezwa mbele

Mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba SC dhidi ya Young Africans SC, uliopangwa kucheza Aprili 9, umesogezwa mbele ambapo sasa utapigwa Aprili 16, 2023 katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetaja sababu za mabadiliko hayo kuwa ni kutokana na uwepo wa tukio la mkutano wa dini Aprili 9, 2023 siku ambayo ilipangwa kwa ajili ya mchezo huo. TPLB imeeleza kuwa mabadiliko ya tarehe ya mchezo huo yameathiri ratiba ya michezo mingine yote ya mzunguko wa 26.

Mabadiliko mengine ni michezo ya mzunguko wa 26 msimu wa 2022/2023 pamoja na michezo mingine miwili ya mzunguko wa 22 kati Geita Gold FC dhidi ya Coastal Union FC .

Aidha, mchezo wa Yanga SC dhidi ya Kagera Sugar uliopangwa kuchezwa Aprili 16, 2023 utachezwa Aprili 7, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Mchezo wa Ihefu FC dhidi ya Simba SC uliopaswa kuchezwa Aprili 15 utachezwa Aprili 8 Uwanja la Highland Estate. Mchezo wa Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ulipangwa kuchezwa Aprili 15, utachezwa Aprili 8, 2023 Azam Complex.

 

Habari Zifananazo

Back to top button