SERIKALI imesema mashirikiano ya kiuchumi na kijamii ya uendelezaji na uboreshaji utendaji kazi katika bandari nchini kati ya Tanzania na Dubai utapunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameliambia Bunge kuwa azimio lililowasilishwa na Serikali bungeni lina manufaa na kwamba mpango huo utapunguza gharama za utumiaji bandari.
“Matokeo yake itaongeza idadi ya meli zitazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 mpaka kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33,” amesema Prof. Mbarawa akiwasilisha Azimio bungeni. ⤵️