Mendy kutua Al Ahli

WAARABU wanaendelea kutikisa dunia ya soka baada ya kipa Edouard Mendy kukaribia kujiunga na Al Ahli ya Saudia Arabia.

Taarifa zinaeleza makubaliano binafsi kati ya klabu hiyo na Msenegali huyo yameafikiwa kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano kama mipango itaenda sawa kama walivyokubaliana kipa huyo wa Chelsea atasaini kunako klabu hiyo.

Kama Mendy atajiunga na timu hiyo, atakuwa mchezaji wa pili kuondoka Chelsea baada ya Kante kutua Al Ittihad.

Habari Zifananazo

Back to top button