Messi afikisha mabao 800

NYOTA wa Argentina, Lionel Messi amefikisha mabao 800 katika maisha yake ya soka baada ya jana kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Panama.

Messi (35) anakuwa mchezaji wa pili kufikia idadi hiyo baada ya Cristiano Ronaldo mwenye mabao 830.

Mabao ya Messi yanajumuisha 672 ya misimu 17 iliyopita akiwa Barcelona na 29 akiwa PSG.

Mabao 99 amefunga akiwa na Argentina, atakuwa na wakati mzuri wa kufunga bao la 100 atakapocheza dhidi ya Curacao.

Messi alifunga bao hilo dakika ya 89 kwa mkwaju wa faulo katika dimba la Monumental Nunez.

Habari Zifananazo

Back to top button