Messi amfunika Ronaldo baada ya mechi 1000

Washambuliaji Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wameendelea kunyukana kwa rekodi licha ya umri wao kuelekea Ukingoni.

Takwimu zinaonyesha katika mchezo wa Argentina na Australia ulikuwa wa 1000 kwa Lionel Messi ambapo kitakwimu amempita mpinzania wake Cristiano Ronaldo alipofikisha michezo 1000.

Baada ya michezo 1000, Ronaldo anasomeka kuwa na mabao 725, pasi za mabao 216, na idadi ya makombe 31. Wakati Messi amefunga mabao 789, pasi za mabao 348 na makombe 41.

Kwa ujumla wake, Ronaldo amefunga mabao 819, katika michezo 1,143 aliyocheza tangu kuanza kwake soka akiwa Sporting Lisbon mpaka sasa ambapo hana timu. Katika michezo hiyo Ronaldo ametoa pasi za mabao 234.

Katika michezo hiyo Ronaldo amecheza dakika 92,796, ambapo amefunga Hatrick 60, penalty 146, ukitoa zile baada ya mchezo kumaliza sare kwa dakika 90 au 30 za nyongeza. Mabao ya faulo ni 58.

Katika mabao yake yote, mabao 141 amefunga kwa kichwa, mabao 151 mguu wa kushoto, na 525 mguu wa kulia, mabao mawili sehemu zingine za mwili.

Kwa upande wa Messi, amecheza dakika 81,995 na kufunga jumla ya mabao yake yote ni 789, amefunga hatrick 56, penalty 105, ukiondoa zile baada ya mchezo kuisha sare au dakika 30 za nyongeza. Amefunga mabao ya faulo 60.

Mabao aliyofunga kwa mguu wa kushoto ni 662, mguu wa kulia ni 98, amefunga mabao ya kichwa 26, sehemu zingine za mwili mabao mawili.

Wawili hao wanaendelea kuchuanao huko Qatar ambapo Kombe la Dunia linaendelea.

Habari Zifananazo

Back to top button