Messi anaingiza $25m kuitangaza Saudia

UNAAMBIWA mkataba kati ya Lionel Messi na Mamlaka ya Utalii Saudi Arabia unampa mshambuliaji huyo wa Argentina Dola milioni 25 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 59, kwa miaka mitatu.

Mkataba huo wa kibiashara, kazi kubwa ya Messi ni kuchapisha vivutio vya Saudia kwenye mitandao ya kijamii hata hivyo baadhi ya likizo zake zitalipiwa na mamlaka hiyo.

Lakini hati hiyo pia ina sharti muhimu kwa maafisa wa Saudi kwamba Messi hawezi kusema chochote ambacho kinaweza kuitia doa Saudi Arabia. Kwa mujibu wa New York Times.

Advertisement

Kwa miaka michache iliyopita, Saudi Arabia imetumia mabilioni kuchukua hisa kubwa katika michezo, ununuzi wa timu ya soka, mechi za ndondi, mbio za magari ya Formula 1 na hivi karibuni kuwekeza kwenye gofu.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *