Messi aumia Miami

MSHAMBULIAJI wa Inter Miami, Lionel Messi alilazimika kufanyiwa mabadiliko dakika 37 baada ya kupata jeraha katika mchezo wa Ligi Kuu ya Marekani (MLS) ulioisha kwa timu hiyo kushinda mabao 4-0 dhidi ya Toronto FC.

Muargentina huyo hakuwepo katika mchezo wa wiki iliyopita ambao Miami ilipochapwa 5-2 na Atlanta.

Imeripotiwa kuwa kuna uwezekano nyota huyo akakosa fainali ya Kombe la US Open dhidi ya Houston Dynamo wiki ijayo.

Meneja wa Miami, Gerardo Martino alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ana jeraha la zamani hivyo ni kama ametoneshwa.

Mshindi huyo mara saba wa Ballon d’Or hakutumiwa na kocha wa Argentina, Lionel Scaloni dhidi ya Bolivia wiki iliyopita.

Mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Jordi Alba pia alipata jeraha dhidi ya Toronto na Martino alisema bila shaka wachezaji wote wawili watakosa mchezo wa Jumapili dhidi ya Orlando City.

“Hakuna nafasi kwao kwa mchezo wa Jumapili,” Martino alisema. Najua tuna fainali Jumatano lakini hawawezi kucheza.”alisema Martino.

Habari Zifananazo

Back to top button