Messi azomewa uwanjani

LIONEL Messi alizomewa na baadhi ya mashabiki wa Paris St-Germain katika mechi yake ya kwanza tangu kusimamishwa kufuatia safari yake ya kiholela nchini Saudi Arabia wakati PSG ilipoichapa Ajaccio 5-0.

Pande zote mbili zilimaliza mchezo zikiwa na wachezaji 10 baada ya Thomas Mangani kumpiga ngumi Achraf Hakimi, ambaye alilipiza kisasi na wote kupewa kadi nyekundu.

Fabian Ruiz na Hakimi walifunga katika kipindi cha kwanza kwa PSG.

Mbappe alifunga mabao mawili mwanzoni mwa kipindi cha pili kabla ya Mohamed Youssouf kujifunga Ajaccio ikishushwa daraja.

Messi alicheza dakika zote 90, akirejea PSG kwa mara ya kwanza tangu afungiwe na klabu hiyo kwa wiki mbili baada ya kusafiri kwenda Saudi Arabia bila ruhusa yao.

PSG ya Christophe Galtier imebakiza pointi nne pekee kuweka rekodi ya taji la 11 la Ufaransa, wako pointi sita mbele ya Lens wanaoshika nafasi ya pili huku mechi tatu zaidi zikisalia.

Habari Zifananazo

Back to top button