Mfahamu Msemaji Mkuu mpya wa Serikali Tanzania – Mobhare Matinyi

DAR ES SALAAM: Julai 2 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Mwanahabari Mobhare Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam. Miezi mitatu baadaye amemteua Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Matinyi mbali na kuwahi kuwa mkufunzi katika Kituo cha Diplomasia cha Musumbiji-Tanzania amekuwa mwanahabari na mchambuzi wa maswala mbalimbali mengi yakilenga kuitetea Tanzania. Pia amewahi kuwa na ukurasa – column katika gazeti la kiingereza la ‘The Citizen’ – The Eagle’s Eye na ameandika Makala mbalimbali kupitia gazeti la Jamhuri.

Wengi wanamkumbuka Matinyi kwa uchambuzi wake tunduizi wa mabendekezo ya Chadema kuhusu Katiba mpya wakati huo akiwa kama Mshauri Mwelekezi huko nchini Marekani.

Hata hivyo, kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya, Mwanahabari huyu kitaaluma, alikuwa akitumika kwenye jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika maarufu kama SADC. Kwa sasa Matinyi anaenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Gerson Msigwa, aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
MAPESA1234567
MAPESA1234567
2 months ago

HE/SHE DIED WITH CARDINAL RUGAMBWA HOSPITAL “CONFERENCE” DISEASE… THE HISTORY OF THIS DISEASE WAS KILLED MORE THAN 5 MILION PEOPLE AROUND THE WORLD MANY WAS CHINESE, EROPEAN, KOREAN AND INDIANS… ALL WHERE WHITE SKIN PEOPLE…. KILICHOBAKI BABA/BWANA YESU ASIFIWE DISEASE

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x