Mfalme Charles III avishwa taji la thamani

MFALME Charles III wa Uingereza na mkewe Camilla wamevishwa taji katika sherehe ya kifahari iliyofanyika Kanisa la Westminster Abbey na Askofu Mkuu wa Jimbo la Canterbury, Justin Welby kuliweka taji la Mtakatifu Edward juu ya kichwa cha Charles III, ikiwa ni sehemu muhimu kwenye ibada ya kutawazwa kwake.

Taji alilovishwa Mfalme Charles III lenye uzito wa kilo mbili limetengenezwa kwa dhahabu na limewekewa idadi ya almasi 2,868, madini ya sapphire 17, Emeralds 11, lulu 269, na madini ya rubi manne.

Miongoni mwa vitu vya thamani vilivyotumika kutengenezea taji hilo ni almasi ya “Cullinan II” ambayo asili yake ni Afrika Kusini na ndio jiwe la almasi kubwa kuwahi kugunduliwa nchini.

Mfalme Charles amekuwa mtawala wa 40 kutawazwa katika tafrija takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Westminster Abbey, tangu mtawala “William the Conqueror” alipopakwa mafuta na kuwa mfalme wa siku ya Krismasi mwaka 1066.

Habari Zifananazo

Back to top button