Mfanyabiashara adakwa kwa udhalilishaji watoto

JESHI la polisi Mkoani Mtwara linamshikilia mwanaume mwenye umri wa miaka 59, mfanyabiashara kwa tuhuma za kulawiti watoto wa kiume wenye umri wa miaka minane.

Akizungumza leo, Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Issa Suleiman, amesema Februari 13 mwaka huu, mtuhumiwa huyo aliwalawiti watoto hao kwa nyakati tofauti baada ya kuwalaghai walipokuwa wakitoka shule.

“Baada ya kupokea taarifa hizo, watoto walipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Ligula kwa ajili ya uchunguzi, ambapo ilibainika kutendewa udhalilishaji huo,” amesema.

Amewataka wananchi mkoani Mtwara kuwa walinzi kwa watoto na kulisaidia jeshi la polisi kubaini wanaofanya ukatili na vitendo vya udhalilishaji kwa watoto.

Habari Zifananazo

Back to top button