IMEELEZWA kuwa watanzania watatumia mfumo wa kuweka fedha kwenye benki za ndani na kuzikuta nchini Malawi, hivyo hivyo kwa raia wa Malawi wataweka nchini kwao na kuzikuta Tanzania ili kuepuka uingizaji wa fedha usio rasmi.
Hayo yameelezwa na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole wakati akizungumza na EA Radio leo Februari 15, 2023.
”Uzoefu niliouona nikiwa Malawi pesa nyingi imekuwa ikiingia katika njia isiyo rasmi ‘black market’ hivyo nchi zote mbili hazinufaiki. Tumezungumza na benki moja hapa Tanzania na Malawi wamekubaliana mfanyabiashara ataweka pesa na kuzikuta upande wa pili.”
Polepole amesema miaka ya nyuma baadhi ya watanzania walikuwa wakifanya biashara na watu wasiowajua hali iliyokuwa ikiwapa changamoto. Amesema Serikali imetengeneza orodha inayotambulika.
“Serikali ya Malawi na Tanzania inawajua kama unataka soya muone flani kama ni mahindi muone flani.” ameongeza Polopole.