Mfumo kupima vipaji vya watoto wazinduliwa

Kwa mara ya kwanza nchini mfumo wa kupima vipaji kwa watoto umezinduliwa rasmi katika Shule ya Sekondari ya Alpha iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mfumo huo utahusika kupima vipaji vya watoto kidijitali, ili kuweza kusaidia watoto kuelekezwa katika vipaji vyao na kuvitumikia ipasavyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mjumbe wa vipaji barani Afrika maarufu kutoka Kenya, Patrice Lumumba amesema watasambaza ujumbe huo mzuri kuwa shule za Alpha ndio zimechaguliwa kuwa kitovu anzilishi kuwa na mfumo huo mpya, ambao utakuwa na manufaa kwa vijana wa kitanzania wa kike na kiume na Afrika pia.

Prof Lumumba ameeleza kuwa kupitia mfumo huo vijana watakaotambulika vipaji vyao watawezeshwa ili mafanikio yao yasikwazwe bali yapewa rutuba.

“Kupitia mfumo huo mtoto atapimwa kipaji chake na kusaidiwa kutumia vizuri kwani kila mtu ana kipaji ila wengine hawajui hivyo hawataweza kutumia ipasavyo kwa kuwa teknolojia sasa ndio kitu muhimu Duniani,”amesisitiza Prof Lumumba.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Alpha Sekondari, James Kabirigi amesema shule hiyo imejikita kugundua vipaji mapema kabla ya mashine hiyo kwa kuanzisha klabu 21 na kufundisha jinsi ya kuwa wajasiriamali.

“Hii mashine ni Watanzania wote kwa hiyo tupo wa aina nyingi wenye uwezo mkubwa,mdogo na amboa hawana watatafutiwa utaratibu,” amesema.

Amesema manufaa yake inamsaidia kupima kipaji na kukijua na kuendelezwa katika shule ya kipaji husika na kusoma kwa haraka na muda mfupi, ili kuweza kutumia kipaji chake.

“Mtoto anapimwa kwa mwanasaikolojia kuchukua historia yake , asili na anapendelea nini baadae anaingia kwenye mashine inachukua vinasaba na wanatoa michoro ambayo inatumwa mtandaoni Geneva wao wanasoma na kurudisha majibu ndani ya dakika chache,”ameeleza Kabarigi.

Amefafanua kuwa watakuwa na kliniki zitakazoendeleza vipaji na pia vyuo na watashirikiana na shirikisho la vipaji duniani na katika kupima wakigundua duniani vipaji hivyo ni vichache atachukuliwa kwenda nje kuendelezwa.

 

Habari Zifananazo

Back to top button