Mfumo mshitiri kumaliza shida ya dawa vituo vya afya

SERIKALI imesema kuwa iwapo Mfumo wa mshitiri (prime Vendor system) ukisimamiwa vizuri utamaliza changamoto ya uhaba wa dawa na Uwepo wa uhakika wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya Nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, George Mmbaga wakati akifungua mafunzo ya wawezeshaji wa mfumo wa mshitiri kwa wataalamu wa maabara,famasia na TEHAMA walioko katika ngazi za Halimashauri mkoani hapa.

Alisema kuwa mfumo huo utawezesha upatikanaji wa bidhaa za afya ambazo zinakosekana Bohari  ya Dawa (MSD) na hivyo kuimarisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma.

“Mafunzo haya ya lengo la kupata wawezeshaji wa mkoa na Halimashauri wa kutumia mfumo lengo ikiwa ni katika vituo vya kutolea kuwepo na upatikanaji wa dawa na vipimo vya kitabibu Ili kuakisi huduma bora kwa wananchi”alisema Mmbaga.

Aidha aliwataka Wakurungezi wa Halimashauri kusimamia makusanyo ya Mapato kwenye vituo vya afya Kwa ajili ya kupata fedha za kutosha Kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za afya sambamba na kusimamia mnyororo wa ugavi wa bidhaa hizo.

Hata hivyo Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Rehema Maggid alisema kuwa serikali imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali Ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya unakuwa kwa asilimia 100.

Habari Zifananazo

Back to top button