Mfumo usaili wa ajira kielektroniki serikalini waiva

Mfumo wa usaili kielektroniki kwa waombaji ajira serikalini, utaanza kutumika mwanzoni mwa mwaka ujao wa fedha, ili kumuwezesha kila mmoja kushiriki akiwa katika mkoa wake.

Mfumo huo umelenga kupunguza, pamoja na mambo mengine, usumbufu na gharama wanazoingia waombaji kwa kulazimika kukusanyika siku kadhaa makao makuu ya nchi kwa mchakato wa usaili.

Naibu Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Samwel Tanguye, amesema leo Aprili 24, 2023 katika mkutano wa ukusanyaji maoni kwa ajili ya kuboresha kanuni za uendeshaji wa shughuli za Sekretarieti kwamba:

Amesema baadhi ya vyuo vya kati, ikiwemo vya ufundi na vya elimu ya juu kila mkoa, vyenye maabara ya kompyuta vitatumika kufanya usaili wa awali ambao ni wa kuandika.

“Sekretarieti itaunganisha mfumo kwenye maabara hizo. Itakua ikituma maswali wakati huohuo wa usaili katika chuo husika, ambapo mwombaji ajira atapata majibu yake hapohapo.

“Watakaopita katika mchujo wa kwanza ndio watakaolazimika kusafiri kwenda Dodoma kwa ajili ya usaili wa mdomo. Tunafanya hivi ili kila mwenye sifa apate nafasi, bila kujali anatoka kwenye familia ya hali gani,” amesema.

Kwa maoni yake Diwani wa Kata ya Bujora wilayani Magu, Bunyanya John, amesema utaratibu uliopo sasa wa uwepo wa nafasi moja tu ya ajira, lakini wanaitwa waombaji zaidi ya hata 500 sio sawa, akaishauri sekretarieti kurekebisha jambo hilo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button