MFUMUKO wa bei nchini Uingereza umepanda hadi asilimia asilimia 11.1 ikiwa ni mara ya kwanza tangu 1981. Huku mfumuko wa bei ya vyakula na vinywaji ukipanda zaidi tangu mwaka 1977.
Hii kwa mujibu wa ofisi ya takwimu ya Waziri wa Fedha.
Kuongezeka kwa bili za nishati ya kaya na bei za vyakula kumefanya mfumuko wa bei wa kupanda ikiwa ni miaka 41 tangu ilipotokea hali hiyo. Taarifa ilionyesha siku moja kabla ya waziri wa fedha, Jeremy Hunt kutangaza kuongezeka kwa ushuru na kupunguza matumizi ili kudhibiti ukuaji wa bei.
Bei za watumiaji zimepanda kwa asilimia 11.1 katika muda wa miezi 12 hadi Oktoba, ni kiwango kikubwa zaidi tangu Oktoba 1981 na kuruka kubwa kutoka asilimia 10.1 mnamo Septemba, Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa ilisema leo.
Awali ilikadiriwa kuwa mfumuko wa bei ungepanda hadi asilimia 13.8 mwezi Oktoba kama serikali isingeingilia kati kupunguza bei ya bili za nishati ya kaya hadi pauni 2,500 ($2,960) kwa mwaka kwa wastani.
Akizungumzia suala hilo Hunt ambaye anatarajiwa kuelezea bajeti mpya siku ya Alhamisi alisema “maamuzi magumu lakini ilibidi wakubaliane na hali hiyo ya kupanda kwa bei.
“Ni jukumu letu kusaidia Benki ya Uingereza katika dhamira yao ya kurudisha mfumuko wa bei kwa lengo kwa kuwajibika kwa fedha za taifa,” alisema katika taarifa.