Mgambo kupewa kipaumbele ulinzi Same

MKUU wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ameutaka uongozi wa halmashauri hiyo na viongozi wengine wa taasisi za umma na binafsi kutoa kipaumbele kwa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Akiba(Mgambo) kuimarisha ulinzi na shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

DC Mgeni amesema hayo jana wakati akihitimisha mafunzo kwa askari 106 wilayani humo akiwataka askari hao kuzingatia kiapo na kuwa mstari wa mbele kupambana na maovu.

“Niwahakikishie vijana wetu serikali itaweka kipaumbele kuhakikisha inapotokea fursa yoyote mnapewa kipaumbele iwe shughuli zilizo chini ya Halmashauri ikiwemo ulinzi, kusimamia makusanyo ya mapato, kukimbiza mwenge na nafasi za JKT mnachopaswa kuzingatia ni uadilifu na kuviishi viapo mlivyo apa baada ya kuhitimu mafunzo”.Alisema mkuu huyo wa wilaya.

Amewataka pia wahitimu hao kuangalia uwezekano wa kuwaendeleza kielimu kwa kusoma kozi mbalimbali ikiwemo udereva, ufundi umeme na uwashi ili kujijengezea ujuzi na sifa za kuwa na vyeti ambavyo vitawasaidia.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button