Mganga mkuu, mfawidhi wahamishwa kituo cha kazi Kahama

Hospitali ya Kahama, mkoani Shinyanga

MKUU wa Mkoa Wa Shinyanga, Chiristina Mndeme ameagiza kuwaondoa kwenye kituo cha kazi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Dk Josephat Shani na Mganga Mfawidhi, Dk Deogratius Nyaga na kuleta madaktari wengine .

Hatua hiyo ni baada ya uzembe uliosababisha kifo cha mama na mtoto ambaye alikaa kwa muda siku mmoja bila kupata huduma licha ya kuwa hospitalini hapo.

Mndeme ameagiza kuletwa haraka Mganga Mkuu na Mfawidi mpya ili kuboresha utendaji kazi wa hospitali hiyo.

Advertisement

“Tumeanza kuchukua hatua kwa baadhi watumishi sita wazembe juu ya kifo hiki naomba katibu Tawala Mkoa , awaondoe watumishi hawa wa ngazi ya juu awapeleke katika wilaya zingine ndani ya mkoa,”alisema Mndeme.

Mndeme amekemea tabia ya baadhi ya Watumishi kujihusisha na vitendo vya rushwa pindi wanapotoa huduma pamoja na matumizi ya sim una kuagiza suala hilo lichukuliwe hatua za kinidhamu kwa watakaobainika.

Mndeme pia amelazimika kuwasimamsha hadharani Watumishi sita waliosababisha mjamzito na kusababisha kifo ambao ni Dk Christina Kulwa, Joyce Shindai, Nuru Philipo, Lemi Majige, Betina Rwamzigwa na Silia Sayenda wote hawa wanadaiwa kumnyima mjamzito huduma ya kujifungua na kusababisha kifo chake na kichanga tumboni.