Mgaya mkuu mpya NIT

ZANZIBAR: RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Dk Prosper Mgaya kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Kabla ya uteuzi huo Mgaya alikua Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus inasema Dk Mgaya anachukua nafasi ya Prof Zakaria Mganilwa ambae amemaliza muda wake.

Taarifa hiyo ya Zuhura inasema uteuzi wa Mgaya umeanza rasmi  juzi Machi 4, 2024

Habari Zifananazo

Back to top button