Mgogoro wa ardhi wa miaka 40 wamalizwa

TANGA:Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amefanikiwa kumaliza Mgogoro wa mpaka uliodumu Kwa miaka 40 kati ya Kijiji cha Kiluwati kilichopo kata vuga Lushoto na vitongoji vya Mwisho wa shamba na Ndulu vilivyopo wilaya ya Korogwe.

Awali maeneo hayo yalikuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu ambapo wilaya ya Lushoto ilikuwa inatambua ni maeneo yake wakati mipaka inaonyesha yapo katika wilaya ya Korogwe.

Akiongea Kindamba mara baada ya kumaliza kikao Cha usuluhishi baina ya viongozi wa pande zote mbili amesema kuwa kuanzia Sasa Kijiji Cha Kiluwati pamoja na vitongoji vya Ndulu na Mwisho wa shamba vitakuwa wilayani Korogwe.

“Ripoti ya wataalamu wa ardhi inaonyesha kwamba maeneo hayo mipaka yake ipo wilayani Korogwe na sio Lushoto kama ambavyo ilikuwa inafahamika hapo awali”amesema RC Kindamba.

Aidha Kamishna wa ardhi mkoa wa Tanga Tumaini Gwakisa amesema chanzo cha mgogoro huo ni uwelewa tofauti wa tafsiri sahihi ya mipaka baina ya wananchi wa maeneo hayo.

Timu ya wataalamu wa ardhi mkoani hapa imejipanga kuendelea kutoa elimu Kwa wananchi juu ya athari za migogoro pamoja na kufanya ukaguzi wa mipaka baina ya wilaya na wilaya na kuweka alama.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
MONEY@
MONEY@
3 days ago

PATA DOLLA $45,000,000 SASA FANYA KAZI NYUMBANI NA HUTAKIWI KUTOKA HATA KIDOGO KABISA

TANGAzo

Chama cha MAPINDUZI kinawatangazia VIJANA WA KITANZANIA 500,000 kuandaa kijiji cha ujamaa eneo la UVUMI DODOMA…

WAHI FURSA HII ADIMU KWA MAENDELEO YA KARNE YA 23

Capture.JPG
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x