Mgombea Misri akutwa na hatia kughushi nyaraka
ALIYEKUWA mgombea urais wa Misri, Ahmed Tantawy amekutwa na hatia ya kughushi nyaraka za uchaguzi na kuamriwa kulipa faini na kuzuiwa kushiriki uchaguzi ujao, vyanzo vinne vya usalama na mahakama vilisema.
Wanachama 21 wa kampeni yake walihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kazi.
Tantawy, ambaye aliibuka kama mmoja wa wapinzani maarufu katika uchaguzi mwaka jana, alijiondoa baada ya kushindwa kupokea saini za kutosha zinazohitajika kuthibitisha kugombea kwake.
Muda mfupi baada ya kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho, alifunguliwa mashtaka ya kughushi nyaraka hizo.
Tantawy Jumanne alihukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja na kuamuru kulipa faini ya pauni 20,000 za Misri.