Mgunda ajitwisha Lawama matokeo Simba

KOCHA Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amesema yeye ndiye anayestaili lawama kufuatia timu hiyo kutolewa mapema kwenye Kombe la Mapinduzi.

Akizungumza na HABARILEO, kocha huyo ameeleza kuwa wachezaji wake walicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi za mabao, lakini walikosa bahati hivyo lawama zote anapaswa kuzibeba yeye na siyo wachezaji.

“Mimi ndi niliyepanga kikosi na mimi ndiye niliyeamua baadhi ya wachezaji kuwapumzisha, ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine ambao hawatumiki mara kwa mara na ni haki yao sababu ni waajiriwa wa Simba na wanapaswa kuitumikia,” amesema Mgunda.

Katika mchezo huo wa Kundi C, Simba ilifungwa bao 1-0 na Mlandege FC kuvuliwa rasmi ubingwa wa michuano hiyo, huku Mlandege ikisonga mbele hatua ya Nusu Fainali, baada ya kumaliza vinara wa kundi hilo kwa kufikisha pointi nne ambazo haziwezi kufikiwa na Simba na KVZ.

Habari Zifananazo

Back to top button