KOCHA Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amesema mchezo wao wa kesho dhidi ya Namungo FC, utakuwa mgumu, lakini wamewaandaa vizuri wachezaji wao kuhakikisha wanapata ushindi.
Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa malengo yao kwa sasa ni kuchukua pointi tatu katika kila mechi watakayocheza na watatumia uzoefu wa wachezaji wao ili kufanikisha malengo yao. Simba imebakisha michezo minne kumaliza ligi.
“Mchezo utakuwa mgumu sababu Namungo wapo nyumbani kwao, lakini tumejipanga kushinda mchezo wa kesho na mingine iliyobaki, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kurudisha ubingwa wetu wa Ligi Kuu msimu huu,” amesema Mgunda.
Kocha huyo ameeleza kuwa baada ya timu yao kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Wydad Casablanca wiki iliyopita, kwa sasa timu hiyo imeweka nguvu zao kwenye mashindano ya ndani ambayo ni Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), ili kubeba mataji hayo msimu huu.
Comments are closed.