KOCHA Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kuhusiana na kuondoka kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, akisema yeye yupo kwa ajili ya kuwapa furaha.
Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa haoni sababu ya mashabiki wao kuwa na presha sababu Robertinho amemwachia programu maalumu za mazoezi mpaka atakaporudi mwishoni mwa mwezi huu.
“Mashabiki wa Simba waondoe hofu kocha amepatwa na matatizo ya kifamilia na atarudi mwishoni mwa mwezi tuliopo tuna maelekezo yote ambayo ametuachia kwa hiyo hakuna kitakachoharibika,” amesema Mgunda.
Robertinho aliondoka nchini Jumatatu wiki hii akielekea kwao Brazil kwa matatizo ya kifamilia na uongozi, umesema kuwa atarudi nchini mwishoni mwa mwezi kuendelea na majukumu yake ya kuifundisha Simba.